Algorithm mpya ya AI kutoka Google inatabiri ugonjwa wa moyo kwa kuangalia macho yako

860

Wanasayansi kutoka Google na kitengo chake cha sayansi Verily wamegundua njia mpya ya kutathmini hatari ya mtu ya ugonjwa wa moyo kwa kutumia mashine ya kujifunza. Kwa kuchambua scans ya nyuma ya jicho la mgonjwa, programu hii ya Google inaweza kutambua data kwa usahihi, ikiwa ni pamoja na kutambua umri wa mtu binafsi, shinikizo la damu, na kama ni wavutaji au la.

Hii inaweza kutumiwa kutabiri hatari ya magonjwa ya moyo – kama vile mshtuko wa moyo (heart-attack) – yenye usahihi sawa na njia za zinazotumika sasa.

Algorithm hiyo inawezesha madaktari kuchambua kwa haraka na rahisi hatari ya magonjwa ya moyo kwa mgonjwa, kutokana na kutohitaji kupima damu. Lakini njia hii inahitaji kufanyiwa majaribio ya kina kabla ya kutumiwa kama njia rasmi ya kutabiri magonjwa ya moyo.
Ingawa wazo la kuangalia macho yako ili kutambua afya ya moyo wako huonekana lisilo wa kawaida, lakini hili linatoka kwenye tafiti zilizo imara. Ukuta wa ndani wa jicho (fundus) umejaa mishipa ya damu ambayo huonyesha afya ya mwili.

Kwa kujifunza muonekano wa mishipa hiyo na kamera na microscope, madaktari wanaweza kutambua vitu kama shinikizo la damu, umri, na kama ni wavutaji, ambayo ni yote muhimu katika utabiri wa afya ya moyo.

picha ya fundus
Picha mbili za fundus, eneo la ndani ya jicho . Picha ya kushoto ikionesha picha ya kawaida: picha ya kushoto ikionesha pichaa kutoka algorithm ya Google ikionesha mishipa ya damu (kijani) kutabiri shinikizo la damu.

Ilipowasilishwa na picha za retina za wagonjwa wawili, mmoja wao ambaye alipata tatzio la moyo kwa miaka mitano iliyopita, na mmoja wao ambaye hajawahi kupata tatizo la moyo, algorithm ya Google iliweza kutambua yupi aliyewahi kupatwa na yupi ambaye hajawahi kupatwa na tatizo kwa asilimia 70.

Hii ni iko chini kidogo ya njia ya kawaida ya SCORE ya kutabiri hatari ya magonjwa ya moyo, ambayo inahitaji mtihani wa damu na hufanya utabiri sahihi katika mtihani huo huo kwa asilimia 72 ya wakati.