Apple iPhone X kufikia tamati mwaka 2018

917

Utabiri wa mchambuzi aliyejulikana kama Ming Chi-Kuo unasema kwamba iPhone X itakabiliwa na “mwisho wa maisha” katika majira ya joto 2018 na haitokua na muendelezo baada ya iPhone mpya kuzinduliwa.

Miezi kadhaa iliyopita kampuni ya Apple ilizindua simu yake iliyokua ikisubiriwa kwa hamu na watu wengi duniani, iPhone X. Simu hiyo ilitengeneza hitaji kubwa kutokana na kuja kwake na design mpya na teknolojia za kushangaza. Hata hivyo iPhone X inaweza ikawa simu ya kwanza ya mwaka uliopita kutoendelezwa mwaka 2018.
Utabiri wa mchambuzi aliyejulikana kama Ming Chi-Kuo unasema kwamba iPhone X itakabiliwa na “mwisho wa maisha” katika majira ya joto 2018 na haitokua na muendelezo baada ya iPhone mpya kuzinduliwa. Huenda labda kwa sababu mauzo ya iPhone ya Apple X hayakuwa ya juu kama ilivyotarajiwa.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka AppleInsider, taarifa ya Ming-Chi Kuo pia imesema kuwa kampuni hiyo itafirisha simu za iPhone X milioni 18 katika nusu ya kwanza ya 2018. Ming-Chi Kuo pia alisema kuwa iPhone X haijafanikiwa nchini China kwa sababu ya notch ambayo imesababishia watumiaji wachache matatizo.

Sio tu hili, Ming-Chi Kuo pia alitabiri kwamba Apple pengine itazindua matoleo matatu mapya ya iPhone mwaka 2018 na matoleo yote yatakuja na full-view display. Toleo moja la bei rafiki litakuja na kioo cha LCD na matole mengine mawili yatakuja na vioo vya OLED.

Unafikiri nini kuhusu hili? Tuachie maoni yako katika sanduku la maoni hapa chini. Asante