Apple: Tatizo jipya la usalama kwa watumiaji wa kompyuta za Mac

1289

Jumanne ilitambulika kwamba kompyuta za Mac zapata tatizo la kiusalama, inakupa uwezo wa kuingia kwenye kompyuta yeyote bila kujaza sehemu ya ‘password’

Apple walizungumza na kusema “Usalama ni jukumu la kwanza kwa kila kifaa au huduma kutoka kwao” na kuomba radhi kwa wote walikumbwa na tatizo hilo na kuzidisha utendaji kazi ili tatizo kama hilo lisijirudie.

Sasa tatizo hilo limetatuliwa, na ‘update’ ya programu kiendeshi ipo tayari. Itajipakua yenyewe bila idhini ya mwenye kompyuta kwa wote wenye programu kiendeshi cha toleo la mwisho (MacOS High Sierra 10.13.1)

Soma Pia: KOMPYUTA: Jinsi ya kuchagua kompyuta itakayofaa kutumia na aina za watumiaji

Kama bado hujapata ‘update’ hiyo, wasiliana na mtaalamu unayemjua wa kompyuta akupe msaada zaidi.