Apple yainunua Shazam kwa dola milioni 400

1361
Apple wainunua Shazam

Kampuni ya Apple wameinunua Shazam, programu ambayo bado ndio njia bora ya kutambua nyimbo ambazo huzifahamu kwa haraka. Mtandao wa TechCrunch ulitoa taarifa za awali za dili hili wiki iliyopita, lakini taarifa hiyo ilithibitishwa na Apple kwa mtandao wa Verge. Mtandao mwingine wa Recode unasema dili hilo lina thamani ya dola za kimarekani, 400 million ($400m), ambayo kwa mujibu wa The Verge ni chini ya dola bilioni 1 ambayo Shazam, ilitathminiwa kua na thamani hiyo mara ya mwisho.

Soma pia: Facebook Messenger yaungana na PayPal kuwezesha ufanyaji malipo

Makampuni yote, Apple na Shazam walitoa taarifa kwa The Verge unayoweza kuipata hapa chini ikianza na ya Apple:

“Tunayo furaha kuwa Shazam na timu yake yenye vipaji wataungana na Apple” Msemaji wa Apple aliiambia The Verge. “Apple Music na Shazam zinashabihiana, wote wana shauku kwa utambuzi wa nyimbo na kuhakikisha kufikisha huduma bora ya muziki kwa watumiaji wetu. Tuna mipango ya kusisimua, na tunatarajia kuungana na Shazam baada ya makubaliano ya leo.”

Na kutoka Shazam:

“Tunayo furaha kutangaza kuwa Shazam imeingia makubaliano ya kuwa sehemu ya Apple”, Shazam walisema kwenye taarifa kwa The Verge. “Shazam ni moja ya programu za juu zaidi duniani na inayopendwa na mamilioni ya watumiaji na hatujaona sehemu bora zaidi ya kutufanya kuendelea kuunda na kuwaridhisha wateja wetu”

Hakuna mipango zaidi iliyoshirikishwa na mpango huo na dili hilo bado linasubiri kukamilika, ingawa kuna uwezekano mkubwa wa kampuni ya Apple kufanikisha dili hilo. The Verge pia waliripoti kua Shazam imekua na wakati mgumu hivi karibuni kupata mapato, wakitengeneza $54 million kwa mwaka 2016.