China yatuhumiwa kufanya udukuzi kwa Umoja wa Afrika

702
Jengo la Umoja wa Afrika
Jengo la Umoja wa Afrika

Serikali ya China ilitoa zawadi za ‘server’ za kompyuta na vifaa vya mawasiliano kwa Umoja wa Afrika miaka mitano iliyopita. Imetuhumiwa kuweka njia ya kuiba data (inserted a backdoor) kwenye mfumo huo wa mawasiliano

Udukuzi huo umejulikana mwezi wa Januari mnamo mwaka 2017, pale wataalam walipoona kati ya saa 6 hadi saa 8 usiku huwa kuna utumikaji wa data za intaneti pale jengo hilo la Umoja wa Afrika likiwa halina watu ambalo lipo mjini Addis Ababa kwenye nchi ya Ethiopia. Baada ya kufanya uchunguzi, ilijulikana shirika hilo linafanyiwa udukuzi na kutuma data zake kwenda mji wa Beijing huko China.

repoti hiyo imetolewa na gazeti la kifaransa Le Monde reported Friday, ingawa uongozi wa China umekanusha tuhuma hizo na kudai hazina ukweli.

Soma Pia: WhatsApp imezuiwa matumizi nchini China, orodha ya mitandao ni zaidi ya 3,000 imezuiwa hadi sasa

Baada ya tuhuma hizo, Umoja wa Afrika umechukua uamuzi wa kununua ‘server’ zao na kukataa msaada wa China walioomba kuzirekebisha ‘server’ za mwanzo, pia umoja huo ulichukua uamuzi wa kupekua jengo zima ili kuondoa vidukuzi vyote.