Datally: Mwokozi wa matumizi yako ya data kutoka Google

1281
Datally - swahilibytes.co.tz

Google imezindua app nyingine katika simu janja za Android na imeundwa kwa lengo la kuweza kudhibiti matumizi ya data kwa watumiaji wake.

App hiyo iliyopewa jina la Datally itaweza kumsaidia mtumiaji kuelewa jinsi data inavyotumika katika simu yake na kuwa na uwezo kudhibiti matumizi ili kupunguza kiasi cha data kinachotumika.

Datally itakuonesha pia apps zinazokula sana data kwenye simu janja yako na kupendekeza njia za kukata matumizi hayo.

Soma Pia: Microsoft Edge sasa kupatikana kwa watumiaji wa Android na iOS

App hiyo kutoka Google pia itakupa ushauri wa huduma bora za Wi-Fi zinazopatikana karibu yako na kukuonesha yenye nguvu zaidi ili uweze kuichagua kuunganisha na simu yako.

Kwa watumiaji wa muda mrefu wa simu janja za Android wanaweza kugundua kuwa vipengele hivi vyote tayari vipo ndani ya simu lakini tatizo ni kuwa vimefichwa sana ndani ya settings na hivyo kumpa shida mtumiaji wa kawaida kuweza kuvifikia.

Datally yenyewe imerahisisha kupata vipengele hivyo kiurahisi na kutumia lugha nyepesi ili kumuwezesha mtumiaji wa kawaida kuweza kutumia.

Unaweza kupakua app hiyo hapa, na kuanza kudhibiti matumizi ya data katika simu yako ya Android mara moja.