Facebook Messenger yafikisha watumiaji 1.3 Billion kila mwezi dunia nzima

981

Watu wengi tunaifahamu programu ya Facebook Messenger inayomilikiwa na kampuni nguli kwa mitandao ya kijamii Facebook, ambayo sasa imefikisha jumla ya watumiaji bilioni 1.3 kila mwezi dunia nzima.

Facebook messenger, programu inayomuwezesha mtumiaji kutuma ujumbe wa papo kwa papo (Instant Messaging) kutoka kwa kampuni nguli ya mitandao ya kimajii ya Facebook, imefikisha jumla ya watumiaji bilioni 1.3 kila mwezi. Hiyo imeifanya Messenger kua moja ya huduma za kimtandao inayotumika zaidi duniani, ingawa bado ipo nyuma ya programu ya kutuma jumbe za papo kwa papo WhatsApp, ambayo pia inamilikiwa na Mark Zuckerberg.

Hatua muhimu kutoka Facebook.

David Marcus, Mtendaji Mkuu wa Facebook  Messenger ameripoti kuhusu taarifa hiyo mpya kwenye ukurasa wake wa Facebook, ambayo pia ametoa maelezo ya hatua hii muhimu kwa kampuni hiyo.

Wakati ikiwa ni kweli kuwa data hizi ni kubwa kutoka kwa programu ya kutuma ujumbe wa papo kwa papo, hatuwezi kukataa yote hii imewezakana moja kwa moja kutokana na kujihusisha kwake na mtandao wa kijamii unaongoza kwa kutumiwa duniani. Wakati mwingine WhatsApp inaendelea kua programu inayoongoza kwa kutumiwa ikiwa na watumiaji bilioni 1.4 kila mwezi duniani.

Ni nini maoni yako kuhusu hili, Tuachie Maoni yako hapo chini!