Facebook Messenger yaungana na PayPal kuwezesha ufanyaji malipo

893

Watumiaji wa mtandao wa kijamii wa Facebook wameongezewa njia mpya ya kufanya malipo kupitia Messenger. Hiyo itawafanya watumiaji wa mtandao huo kuweza kulipana kwa njia ya PayPal.

Kuweza kutumia huduma hiyo, utaanzisha malipo kwa njia iliyokuwa ikitumika, kwa kubofya “+” na kisha kuchagua kitufe cha kijani cha malipo. Ukishaweka kiasi cha pesa utabofya “pay” na utaletewa njia za kufanya malipo yako, ambayo kwa sasa itakuwa na PayPal kama mojawapo ya njia za kutuma pesa.

Soma Pia: Hyatt: Shirika kubwa la hoteli duniani limeibiwa data za malipo(Visa card & Mastercard) na wadukuzi

Njia hii ni nzuri kwa wale ambao tayari washakuwa na mazoea ya kufanya malipo kupitia PayPal na pia kwa wale wasiopenda kutoa taarifa za kadi zao za debit katika mtandao wa Facebook.

Hata hivyo kipengele hicho kinapatikana tu kwa watumiaji wa iOS nchini Marekani, lakini pia kitawasili kwa watumiaji wa Android hivi karibuni.