Facebook yapata kashfa nzito kuhusu uchaguzi mkuu wa Kenya

710
Uchaguzi mkuu Kenya 2013
Uchaguzi mkuu Kenya 2013

Kampuni inayomiliki mitandao mikubwa ya kijamii (Facebook, Instagram na WhatsApp) imepata kashfa nzito ambayo imesababisha kupoteza thamani yake katika soko kwa dola bilioni 50 kwa kuruhusu Profesa wa chuo kikuu cha Cambridge Aleksandr Kogan na kumpa uwezo wa kuchimba data (jina lako, umri, picha, vitu unavyopenda, mahali ulipo, marafiki wako na vyote kuhusu wao)

Kwa kipindi hicho ilikua sio kinyume na sheria za Facebook kuchukua data hizo, ila Profesa huyo kwa kuvunja sheria aliwauzia kampuni ya Cambridge Analytica data hizo za watu milioni 50

Cambridge Analytica ni kampuni inayohusika na kutengeneza njia na taaluma za kushawishi wapiga kura kuchagua kiongozi. Mnamo siku ya jumatatu tarehe 19 machi mwaka huu, Television iitwayo Channel4 ya huko Ulaya ilionyesha Video ya mkurugenzi mtendaji Alexander Nix akiongea kuhusu njia za rushwa na kutumia wanawake katika kushawishi na kumpa kashfa mwanasiasi mpinzani wa mteja wao katika uchaguzi.

Katika Video hiyo, Cambridge Analytica imesema ilisimamia uchaguzi wa Raisi Uhuru Kenyatta katika kampeni mbili za mwaka 2013 na 2017, wakielezea waliandika maneno ya kuongea na kusimamia utambulisho wote wa kampeni zake, jinsi walivyochafua kiongozi mpinzani.

Hayo yote na zaidi waliweza kuyafanya kwa kutumia mitandao ya kijamii na data za facebook, na kusambaza propaganda za uongo na kumchafua kiongozi wa chama pinzani Raila Odinga

Soma Pia: China yatuhumiwa kufanya udukuzi kwa Umoja wa Afrika

Angalia video hiyo iliyorekodiwa kwa siri jinsi wakielezea utaalam wao kuhusu uchaguzi na propaganda za uongo  kwenye uchaguzi wa marekani hadi walizofanya nchini Kenya. Anza kuangalia dakika ya 5:40

Soma Pia: Microsoft kumpa vifaa mwalimu wa Ghana anaefundisha kompyuta ubaoni

Mpaka sasa Facebook hawajatoa jibu lolote kusuhusu kashfa hizo, zaidi ya kusema iliwaambia Cambridge Analytica wafute data hizo mnamo mwaka 2015.

Tuandikie maoni yako kuhusu habari kwenye comment

Ongea na mimi kuhusu teknolojia kwenye Twitter yangu, nitakujibu!