Facebook yafuta akaunti feki milioni 583 katika kipindi cha miezi mitatu

400
Facebook akaunti keki

Huenda mtandao wa kijamii wa Facebook upo katika mchakato wa kujisafisha mara baada ya kashfa nzito iliyopata siku za hivi karibuni.

Facebook imesemekana kufuta akaunti feki za watu takribani milioni 583 katika kipindi cha miezi mitatu ya mwaka huu wa 2018 kwenye ripoti iliyoitoa hapo jana.

Mtandao huo wa kijamii ulitoa kwa mara ya kwanza ripoti hiyo hapo Jumanne ikielezea idadi ya machapisho pamoja na akaunti feki ilizofuta katika robo ya kwanza ya mwaka 2018.

Pia imekadiriwa kuwa yapata zaidi ya majaribio milioni 6.5 yamefanyika kwenye utengenezaji wa akaunti feki katika mtandao huo kuanzia Januari 1 mpaka Machi 31 mwaka huu.

Uendeshaji wa akaunti feki pamoja na machapisho yenye kujiendesha yenyewe yanafanyika pia kwenye mitandao mengine mashuhuri kama Twitter na YouTube. Ripoti moja iliyotolewa mwezi Aprili mwaka huu ilisema theluthi mbili ya links zinazotumwa Twitter zilitoka kwa bots (akaunti roboti).