Filamu 10 zilizoongoza kupakuliwa kupitia torrent katika wiki

  862
  upakuaji haramu

  Kwa kipindi cha muda mrefu sasa watu wengi hutumia mitandao tofauti ya torrent kupakua vitu mbalimbali ikiwemo filamu, vitabu vya kielektroniki, miziki n.k.

  Licha ya kuwa ni njia haramu ya kupakua vitu hivyo lakini pengine ndio njia inayotumiwa na wengi kutokana na changamoto za kulipia mitandao inayotoa huduma hizo kihalali kama vile Netflix, Hulu, na iTunes.

  Soma Pia: Instagram sasa yaruhusu watu wawili kwenda mubashara ‘Live’ kwa wakati mmoja

  Tovuti ya TorrentFreak imetoa orodha ya filamu zilizoongoza kupakuliwa zaidi kwa njia ya torrent katika juma lililopita.

  TorrentFreak hutumia makadirio kupata idadi ya namba filamu moja hupakuliwa na kisha kuandaa orodha kila wiki.

  Orodha ya filamu hizo ni kama inavyoonekana hapo chini:

  1. Spider-Man: Homecoming
  2. War for the Planet of the Apes
  3. Baby Driver
  4. Pirates of the Caribbean: Dead Men Tell No Tales
  5. Transformers: The Last Knight
  6. 6 Days
  7. Wonder Woman
  8. Despicable Me 3
  9. The Dark Tower
  10. Hitman’s Bodyguard