Gari la Uber linalojiendesha limegonga na kuua mtembea kwa miguu

791

Gari la Uber huko kwenye mji wa Arizona Nchini Marekani, limegonga mwanamke aliyekua anatembea kwa miguu kwenye sehemu ya kuvukia na kumuua

Gari hilo la Uber lilikua kwenye mfumo wa kujiendesha lenyewe, dereva wa ndani alikua haendeshi. Mwanamke alikua akivuka barabara baada ya kugongwa alifia njiani akipelekwa hospitalini kutokana na majeraha makubwa.

Uber wanashirikiana na polisi kwenye uchunguzi wa ajali hiyo na hii ndo kauli yao kwenda kwa polisi

Mji wa Arizona umekua ukipata majanga mengi kwa watembea kwa miguu huko nchini marekani. Hii ni mara ya kwanza kwa gari la kujiendesha lenyewe limegonga na kuua, Kampuni ya Uber imesimamisha huduma zote za magari yenye teknolojia ya kujiendesha yenyewe, ambayo ilikua ikiyafanyia majaribio katika teknolojia hiyo.

Soma Pia: Tigo yaungana na Selcom na Mastercard kuleta huduma ya Mastercard QR Tanzania

Karibu kwenye Twitter yangu tuongee kuhusu teknolojia, nitakujibu!