Google, Facebook, Twitter na Microsoft waungana kwenye mradi wa Data Transfer Protocol

151

Siku ya ijumaa, Google, Facebook, Twitter na Microsoft watangaza nia yao kwa pamoja kujihusisha na mradi wa Data Transfer Protocol unaotengenezwa ili kuwezesha njia rahisi ya kuhamisha Data kwenda sehemu tofauti za ‘platforms’ zao bila hitaji la kupakua na kupandisha data kila mara mtumiaji anapohama kwenda ‘platform’ nyingine.

Mpaka sasa mfumo huo wa Data Transfer Protocol unaweza kuhamisha Data kama picha, barua pepe, anwani, kalenda na notes, kutoka kwenye mahala kama Google, Microsoft, Twitter, Flickr, Instagram, Remember the Milk, na SmugMug.

Soma Pia: Wezi waiba iPhone zenye thamani ya $19,000 kwenye duka la Apple

Microsoft wameelezea kwenye chapisho la blogu yao na kuomba kampuni nyingine ziungane kuendeleza mpango huo ili mbele kuwe na mabadiliko mazuri ya jinsi Data zinavyotunzwa na kuhamishwa. Mfumo huo upo Github kwa yeyote atakaeoenda kuangalia unavyotengenezwa.

Ongea na mimi kwenye Twitter!