Google ipo karibuni kulipa faini kubwa kwa kuvunja sheria za Umoja wa Ulaya

196

Kampuni kubwa duniani ya Google inayoongoza katika uwanja wa huduma za kwenye intaneti na kumiliki mfumo wa Android, YouTube, Google Search, Chrome, Gmail na zaidi, ipo hatiani kwa makosa ya ushindani kibiashara kwenye mfumo wa Android unaoongoza kutumiwa kwenye simu janja.

Umoja wa Ulaya waliweka sheria za ‘anti-trust law’ ili kuwezesha ushindani katika biashara kati ya makampuni kwa wapewa huduma.

Baadhi ya sheria ambazo Google wapo hatiani ni kulazimisha watengenezaji simu zote za Android kama Samsung, HTC, Sony, Huawei waweke programu za Google Search na Chrome kama chagua la kwanza katika kutumia huduma za kutafuta kwenye intaneti. Ya pili ni Google kuwazuia hao watengenezaji simu kuuza simu nyingine zenye programu kiendeshi (Operating System) tofauti na Android. Pia kuwapa motisha ya fedha ili waendelee kuweka huduma za Google kuwa namba moja katika simu hizo. Ikikadiriwa faini ya Google itakua dola bilioni $5, ingawa Google wapo kwenye kupambana na kesi hiyo inayowashikilia shingoni.

Uchunguzi ulianza kufanywa mnamo mwaka 2017 na Margrethe Vestager

Source: TNW

Ongea na mimi kwenye Twitter!