Google waleta app mbadala wa Android Pay na Google Wallet

624

Kampuni kubwa ya kiteknolojia, Google, imezindua application mpya kwa ajili ya matumizi ya malipo kupitia mtandao iitwayo Google Pay.

Kuwasili kwa app hiyo mpya ina maana matumizi ya Android Pay na Google Wallet yamefikia kikomo, hiyo ni kutokana na Google Pay kujumuisha matumizi ya apps hizo mbili za zamani katika app hiyo mpya.

Google Pay katika simu ya Pixel 2

Google wana mipango mikubwa juu ya Google Pay, huku kampuni ikiahidi kuwa huduma zake zitazifikia bidhaa zingine za Google, zikiwemo Chrome na Assistant.

Kujua mengi kuhusu application hiyo mpya, bofya hapa.