Google yakubali kununua sehemu ya HTC kwa dola bil 1.1

873
Makao makuu ya Google
Makao makuu ya Google

Hii imetokana na Google kuwa na changamoto kubwa kwa kipindi chote ya kutokua na kitengo cha ‘hardware’ kwa upande wa simu janja ‘smartphone’

Google wamekua watengenezaji wakubwa wa mfumo wa uendeshaji ‘operating system’ maarufu kama Android, lakini wamekua wakitumia huo mfumo kwenye kampuni za wengine kama Samsung, LG, Huawei na wengineo.

Kutokana na changamoto hiyo ya kushindwa kutumia simu zao wenyewe huku wakiwa na matoleo kama Google Nexus na Google Pixel, lakini bado sio ‘hardware zao’ wameamua kuchukua hatua ya manunuzi ya HTC kwa bilioni 1.1 na kuchukua wafanyakazi 2000 wa uhandisi.

Ushindani na soko la simu janja

Hadi leo kampuni ya apple imekua ikiongoza kwa faida kwenye soko la simu janja, na Google wamekua na wakati mgumu kwenye kushindana na soko la iPhone. Ila kununua HTC inawekezana ikawa ni jambo zuri, kwasababu Google wataweza kutoa simu zao kiwandani na kuweka ‘operating system’ ya Android kwa ubunifu zaidi kulingana na ‘hardware’ watakazopendelea.

Ushindani wa simu janja

 

3 COMMENTS

Comments are closed.