Google yaanza kuruhusu malipo ya M-pesa kwenye Google Play

900
google-mpesa

Kwa kipindi kirefu hapo nyuma, wanunuzi walikua wanaweza kutumia kadi tu kufanya malipo, hatua ambayo iliwafanya wanunuzi wengi kushindwa kutumia Google Play.

Nairobi,Kenya- Kampuni ya kimataifa inayowezesha manunuzi ya mtandaoni, DOMOCO Digital imeshirikiana na SafariCom kuwapa wateja chaguo la kununua bidhaa kwenye soko la Google (Google Playstore) kwa kutumia M-Pesa.

Hatua hii, ambayo inawezeshwa na kampuni ya DOCOMO Digital kwa kutumia API ya malipo ya Google Play, inaruhusu wateja wa M-Pesa kutumia huduma ya fedha za simu ili kulipia bidhaa na huduma kutoka kwenye store ya Google Play.

Huduma inapatikana kwa wateja zaidi ya milioni 27 wa M-Pesa nchini Kenya wenye Android, kwa simu janja au tablet.

Kwa kipindi kirefu hapo nyuma, wanunuzi walikua wanaweza kutumia kadi tu kufanya malipo, hatua ambayo iliwafanya wanunuzi wengi kushindwa kutumia Google Play.

Hatua hii, inaunganisha Google Play na urahisi wa kufanya manunuzi kwa M-pesa ambao watumiaji wengi wameshauzoea wanaponunua bidhaa na huduma. Hii inafanya Google Play kua mtandao wa kwanza wa kufanya manunuzi mtandaoni (e-commerce) kuruhusu miamala ya simu (mobile money).

Hatua hii itasaidia sana kurahisisha ufanyaji manunuzi kwenye Play Store, je nini maoni yako kuhusu hili. Tuambie hapo chini.