Huawei wamekuja na Nova 2i yenye kamera 4 na kioo chenye uwiano wa 18:9

860

Hivi karibuni kampuni ya Huawei imetambulisha toleo lake jipya la simu janja iliyopewa jina la Nova 2i ikiwa ni muendelezo wa toleo lililopita la Nova 2. Simu hii inakuja na jumla ya kamera 4 ikiwa na kamera mbili za mbele na mbili za nyuma.

 

Huawei wamekuja na Nova 2i yenye kamera 4 na kioo chenye uwiano wa 18:9 (Full View Display)

Hivi karibuni kampuni ya simu ya Huawei imetangaza toleo jipya la simu janja iliyopewa jina la Nova 2i. Tole hili jipya lina skrini ya Full View ikiwa na eneo kubwa la skrini na nafasi ndogo ya kuta za pembeni (bevels). Lakini hilo sio jambo pekee linalofanya simu hii kua ya kuvutia. Huawei Nova 2i pia inakuja na kamera mbili kila upande mbele na nyuma (dua cameras).

Muonekano (design) wa Huawei Nova 2i ni jambo lingine la kuvutia kutoka kwenye simu hii. Ni nyembamba sana (7.5mm ) na imefunikwa na umbo la metallic. Teknolojia ya kusoma alamza za vidole (fingerprint reader) imewekwa nyuma ya simu. Na zaidi simu hii inakuja na prosesa ya Kirin 659, 4GB za RAM, ujazo (storage) wa 64GB pamoja na battery yenye uwezo wa 3,340 mAh.

Sifa kamili za Huawei Nova 2i

Kioo: 5.99-inch IPS FullHD, 2.5D Crystal, Full View

Kamera ya Nyuma: Dual 16 + 2 Megapixel Dual-Tone Flash

Kamera ya Mbele: Dual 13 + 2 megapixels with flash, f/2.0

Ujazo wa ndani: 64GB

Ujazo wa ziada: microSD hadi 256GB

Prosesa na RAM: Kirin 659 Octa-Core na 4GB RAM

Battery: 3340 mAh

Mfumo wa Uendeshaji: Android 7.0 Nougat

Connections: VoLTE, NFC, Bluetooth 4.2, WiFi, GPS, LTE, nanoSIM

Uwezo wa ziada: Fingerprint reader, knuckle gestures

Bei: Inakadiriwa kati ya $350 (Tsh 790,000/-)