Hyatt: Shirika kubwa la hoteli duniani limeibiwa data za malipo(Visa card & Mastercard) na wadukuzu

  847

  Hyatt imetangaza hapo jana kuthibitisha tukio hilo, kwa kusema data zilizoibiwa ni za malipo ya kadi (Visa card & Mastercard), takribani hoteli 41 katika nchi 11. Kuibiwa huko kulijulikana mnomo mwezi Julai, na taarifa za upelelezi kukamilika.

  Katika taarifa hiyo, wameelezea data zilizoibiwa ni namba za kadi, tarehe ya kuisha kadi,na namba tatu za usalama, hivyo vyote vinawatosha wadukuzi hao kutumia pesa zako kwa malipo ya Visa au Mastercard bila kujulikana. Udukuzi kama huo ulitokea mwaka 2015 pia ndani ya shirika hilo, wakatoa maelezo na kusema wataongeza ulinzi zaidi.

  Soma pia: WhatsApp imezuiwa matumizi nchini China, orodha ya mitandao ni zaidi ya 3,000 imezuiwa hadi sasa

  Kama ulitumia kadi yako kwenye hotel hizo za Hyatt kuanzia mwezi wa 3 hadi wa 7, kuwa makini kuangalia utumiaji wa hela zako kama kuna udukuzi wowote usioujua. Hyatt hawajajua ni wateja gani ambao wapo hatarini na imeshindwa kutuma ujumbe wa email kuwataarifu. Ni jukumu letu kufatilia utumiaji wa kadi zetu.

  Angalia orodha ya hoteli zilizoathirika

  Ahsante kwa kusoma, tuachie maoni yako.