Instagram Lite yazinduliwa kwa watumiaji wa Android

127
instagram lite

Instagram imefuata nyayo za kampuni baba Facebook kwa kuzindua toleo jepesi (lightweight) la programu yake na sasa linapatikana rasmi Google Play.

Kama ilivyo kwa Facebook Lite, Instagram Lite imetengenezwa kwa ajili ya watumiaji wa simu janja zisizo na uwezo mkubwa hususani katika nchi zinazoendelea, na itapatikana kwa uwezo kilobytes 573 badala ya megabytes 32 za programu kuu.

SOMA PIA: Vipengele 10 vya muhimu kwenye iOS 12 inayokuja hivi karibuni

Uwezo mdogo wa programu hiyo kutawezesha watumiaji wake kutumia hata kukiwa na mawasiliano hafifu ya intaneti.

Kupitia Instagram Lite watumiaji wataweza kutuma na kuangalia picha pamoja na stori, wataweza pia kutumia kipengele cha Explore. Watumiaji watashindwa kushea video na kupokea ujumbe wa moja kwa moja (direct message) ili kuweza kuokoa nafasi ya kuhifadhi vitu katika simu.