Instagram sasa yaruhusu watu wawili kwenda mubashara ‘Live’ kwa wakati mmoja

815

Siku za hivi karibuni mtandao wa kijamii wa Instagram umetangaza kufanya majaribio ya kipengele (feature) chao kipya kitakacho ruhusu watumiaji wawili kwenda mubashara kwa wakati mmoja.

Kwa maana nyepesi zaidi hii haimaanishi kwenda mubashara na rafiki uliyekua nae ndani ya chumba kimoja, hii ina maanisha unaweza kumualika hata rafiki yako aliye upande tofauti na wewe wa dunia kujiunga kwa kutumia kifaa chake.

Unapomualika mtu kujiunga na mubashara na wewe, skrini itagawanyika mara mbili na rafiki yako ataungana na wewe kwenye upande wa pili wa skrini. Watazamaji wataweza kuendelea kutazama na kuacha maoni kama kawaida.

Soma Pia: Twitter yaongeza mara mbili kiwango cha maneno katika tweet

Cha kuvutia zaidi kuhusu kipengele hiki ni uwezo wa kumuondoa na kumuweka rafiki yako yoyote mwingine wakati ukiendele kua mubashara.

Kwa mujibu wa Instagram, kipengele hiki bado kinafanyiwa majaribio na watumiaji wachache na inategemea kuachiwa kwa watumiaji wote miezi kadhaa ijayo.

Chanzo: Instagram Blog

Ni nini maoni yako kuhusu kipengele hiki kipya, Tuachie Maoni yako hapo chini!