Instagram yazindua programu ya IGTV kwa watumiaji

311

Katika kipindi cha miaka nane iliyopita, watumiaji wa Instagram wamekuwa wamezoea kuvinjari picha, memes, na video fupi fupi katika programu ya Instagram. Lakini siku ya Jumatano, Juni 20, programu ya kushare picha (Instagram) ilitangaza kipengele kipya ambacho kitaleta ushindani wa moja kwa moja na YouTube, Vimeo, na tovuti nyingine za kusambaza video.

Huenda ukawa unashangaa IGTV ni nini?,

Bila shaka unapaswa kupata msisimko juu yake, kwa sababu ni dhahiri itabadili jinsi unavyoutumia mtandao wa Instagram. Watumiaji sasa wataweza kupakia video za wima (vertical) ambazo zina urefu wa hadi saa moja, kinyume na video za zamani za video za muda mfupi (dakika 1), na hii italeta mapinduzi ya jukwaa hilo kwa watumiaji ulimwenguni kote. Hata kama huna nia ya kutengeneza kitu chochote peke yako, kuna nafasi kubwa sana ya kufurahia hili.

Kwa taarifa zilizotolewa, IGTV itakuwa na programu yake ya kujitegemea. Hata hivyo, watumiaji bado wataweza kuangalia video za IGTV kutoka kwa Instagram pia, kwa kubonyeza kitufe juu ya home skrini ya Instagram, ambayo kimekaa kama televisheni ya zamani.

SOMA PIA: YOUTUBE: Video 10 za Tanzania zinazotamba kwa views mpaka sasa

Usiwe na shauku sana hata hivyo, kwa sababu kipengele hiki (na programu ya IGTV) haitakuwa inapatikana mara moja kwa watu wengine. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Instagram, IGTV itatoka duniani kote ndani ya wiki chache zijazo kwenye vifaa vya Android na IOS.