iPhone X: Hiki ndo kionjo kipya cha Animoji kinachopendwa sana

764

Hapo mwezi wa Septemba, Apple walitambulisha simu mpya za iPhone ambazo ni iPhone 8, iPhone 8 Plus na iPhone X. Katika utambulizi huo walielezea vionjo vyote vipya utakavyokuta ukitumia simu hizo.

Animoji ni kionjo cha iPhone X ambacho kinakupa uwezo wa kuonyesha ishara za uso (Facial expressions) kama kuongea, tabasamu, hasira, huzuni, na kufatiliza mdomo wako. Hayo yote yanafanyika kwa kutumia camera ya mbele inayosoma uso wako na kuipa Animoji ishara zote.

Watu wengi kwenye mitandao ya kijamii wameonyesha kupendezwa na kionjo hiko, na kutumia Animoji kwenye nyimbo kama Gasolina, Despacito, Man’s Not Hot na zaidi

Pia soma: Sifa 5 utazikuta kwenye matoleo yote ya iPhone X, iPhone 8 na iPhone 8 plus

Wakati huo huo Samsung wapo kwenye matengenezo ya Samsung Galaxy S9, ambayo inatolewa ifikapo mwezi wa 3 mwakani, wakiwa na dhumuni la kuifunika iPhone mpya katika ubora, vionjo na mauzo. Usisite kutuandikia maoni yako.