Jeff Bezos ni mtu tajiri zaidi duniani, utajiri wake wafikia $150 billioni

204
(Photo by Michael Tullberg/WireImage)

Utajiri ya muanzilishi wa Amazon.com Inc sasa umefikia $150 bilioni huko New York, Jumatatu hii, kwa mujibu wa Ripoti ya Bloomberg Billionaires. Hiyo ni zaidi ya dola bilioni 55 za utajiri Bill Gates , muanzilishi wa Microsoft Corp, tajiri wa pili wa dunia.

Bezos anakua tajiri zaidi katika historia ya kisasa baada ya kupita makaridio ya mfumuko wa bei aliofanyiwa Bill Gates. Mwaka 1999, Bill Gates aliwahi kufikia utajiri wa dola billion 100 kwa muda mchache, na anakadiriwa angekua na utajiri wa dola bilioni 149 kwa thamani ya dola ya sasa.

SOMA PIA: Jua ‘updates’ za programu za mitandao ya kijamii kwenye simu janja

Hiyo inafanya Bezos kua tajiri zaidi kuliko mtu mwingine yeyote tangu angalau 1982, wakati Forbes ilichapisha taarifa za watu matajiri kwa mara ya kwanza.

Bezos amefikia alama ya utajiri wa Dola bilioni 150, siku ambayo kampuni za Amazon ilianza kampeni ya Prime Day, tukio lao kubwa la mauzo la kila mwaka duniani.
Hisa za Amazon.com zimeongezeka kwa siku nane za mfululizo na na kufikia $9.46, au 0.5% Jumatatu na kufunga katika rekodi ya $1,822.49.

Soko la Amazon limeongezeka kwa zaidi ya 55% kwa kipindi cha chini ya miezi saba, kitu kilichosababisha utajiri wa Jeff Bezos kuongezeka kwa zaidi ya dola bilioni 50 katika kipindi hicho.

Orodha ya kumi bora ya matajiri wa dunia:

List ya matajiri kumi wanaoongoza duniani