Jinsi ya kufanya ‘Factory Reset’ simu janja zote za android zenye password au pattern

1437

Ukiwa umesahau password yako au pattern ya simu janja, mara nyingi huwa tunapeleka simu kwa fundi ambae tunamjua atusaidie. Nimekuletea njia rahisi ya kufanya ‘Factory reset’ mwenyewe

 

Kabla ya yote, jua kwamba data na faili zako kama namba za simu, picha, apps na vitu vyote vitafutika baada ya kufanya factory reset. SwahiliBytes haitahusika na ufutaji huo, fanya kwa tahadhari.

 

Simu za Samsung

Hatua 1: Bonyeza kwa pamoja kwa sekunde 7

Sauti juu + Kitufe cha kuzimia + Kitufe cha nyumbani

Hatua 2: Zitakuja orodha mbali mbali, kwa kutumia vitufe vya sauti shuka chini hadi kwenye “wipe data / factory reset”

Hatua 3: Bonyeza kitufe cha kuzimia simu (power). Itakuja orodha nyingine, shuka chini kwa kutumia kitufe cha sauti na chagua “Yes — delete all user data”. Hapo itakua tayari imefuta kila kitu.

 

Simu za Huawei

Hatua 1: Bonyeza Sauti chini + Kitufe cha kuzimia + Kitufe cha nyumbani kwa pamoja kwa sekunde 10

Hatua 2: Zitakuja orodha mbali mbali, kwa kutumia vitufe vya sauti shuka chini hadi kwenye “wipe data / factory reset”

Hatua 3: Bonyeza kitufe cha kuzimia simu (power). itakuja orodha nyingine chagua “Yes — delete all user data”. Hapo itakua tayari imefuta kila kitu

 

Simu za Tecno

Hatua 1: Bonyeza Sauti juu + Kitufe cha kuzimia kwa pamoja hadi logo ya android itokee

Hatua 2: Ikitokea logo achia vitufe hivyo, na bonyeza tena mara moja bila kushikilia ‘Sauti juu + Kitufe cha kuzimia’

Hatua 3: itakuja orodha, shuka kwa kitufe cha sauti hadi kwenye “Wipe data / factory reset” na kisha bonyeza kitufe cha kuzimia simu (power). itakuja orodha nyingine chagua “Yes — delete all user data”. Hapo itakua tayari imefuta kila kitu.

Simu za HTC

Hatua 1: Bonyeza Sauti chini, na bila kuachia bonyeza pia Kitufe cha kuzimia hadi logo ya android itokee

Hatua 2: zitakuja orodha mbali mbali, kwa kutumia vitufe vya sauti shuka chini hadi kwenye “wipe data / factory reset”

Hatua 3: kisha bonyeza kitufe cha kuzimia simu (power). itakuja orodha nyingine chagua “Yes — delete all user data”. Hapo itakua tayari imefuta kila kitu.

 

Soma Pia

  1. Jinsi ya kuangalia movie mtandaoni bila kuipakua
  2. Jinsi ya kupakua video kutoka Youtube kwa simu janja na kompyuta zote

 

Simu za LG

Hatua 1: Bonyeza Sauti chini, na bila kuachia bonyeza pia Kitufe cha kuzimia hadi logo ya android itokee

Hatua 2: Logo ya android ikitokea, achia kitufe cha kuzimia simu janja hiyo, endelea kubonyeza Sauti chini kwa sekunde 2

Hatua 3: Bonyeza kitufe cha kuzimia simu mara moja, ikitokea skrini nyingine ya factory reset, achia kitufe cha hatua 2

Hatua 4: Tumia kitufe cha sauti chini kuchagua Yes

Kama una swali au maoni, tuandikie kwenye comment chini na tutakujibu, ahsante!