Jinsi ya kutatua tatizo la NO BOOTABLE DEVICE FOUND kwenye computer yako

1208

Hili ni tatizo limetukuta watumiaji wengi sana wa computer, unawasha computer kasha inatokea screen nyeusi ikionyesha maneno “Bootable usb not found” unaweza ukazani labda komputa yako eitha hard disk au programu kiendeshi(window) imeharibika.

Ukiona tatizo hilo usiogope sana bali jaribu kufanya vitu vifuatavyo ili kujua kinachosababisa tatizo hilo.

Angalia kama umechomeka flash, external hard drive au kuna cd.

Mara nyingi sana watu huwa wanawasha komputa zao huku flash, external hard drive  imechomekwa, komputa ikiwa inawaka inafanya Power On Test(POST). inaangalia isome programu kiendeshi toka kwenye chombo gani usb au cd, kama hicho chombo hakina programu kiendeshi itakuletea iyo messeji ya NO BOOTABLE DEVICE FOUND

kwa hiyo ili kuepukana na tatizo hili hakikisha kua Komputa yako haijachomekwa flash au external hard disk kabla ya kuwasha.