Jinsi ya kutumia ‘Gmail’ moja na watu wengine bila kuwapa ‘password’

994

Pengine wewe ni mtu mwenye ‘password’ moja kila mahala, na una barua pepe ya biashara ambayo unahitaji kutumia na watu, ili mpate email wote. Unaweza kuongeza watu 10 wapate barua pepe za ‘account’ yako

Pengine wewe ni mfanya biashara, hii ni muhimu sana katika kuhudumia wateja wako. Utakao waongeza kwenye barua pepe yako wataweza kutuma, kupokea na kufuta barua pepe ila hawataruhusiwa kubadilisha ‘password’ yako

Jinsi ya kuongeza watumiaji

  1. Nenda kwenye ‘Settings’
Account yako ya Gmail
Account yako ya Gmail

Soma pia: Twitter yaongeza mara mbili kiwango cha maneno katika tweet

2. Chagua ‘Accounts and Import’

3. Chagua ‘Add another account’

4. Ingiza email ya Gmail unayotaka ipate ruhusa

Mruhusiwa atapata ujumbe wa barua pepe ambayo anatakiwa akubali ndani ya siku 7.

Kwa njia hizo chache utaweza kupunguza usumbufu wa hapa na pale kuhusu barua pepe za kikazi, na kutoa huduma kwa wateja vizuri kwa kushiriakiana na wengine

Usisahau kushare na wanaohitaji huu ujuzi, pia toa maoni yako ni kipi ungependa kujua au kuongezea. Thank you!