Jinsi ya kuzima ‘Last Online’ kwenye Instagram

831

Leo tutatazama jinsi ya kuzima “Last Online”, kipengele kipya kilichotambulishwa na mtandao wa Instagram majuma kadhaa yaliyopita. Njia hii itakuwezesha kuzima ‘last online’ ili watu wasione mara ya mwisho kuwa online ilikua saa ngapi, angalia mwongozo kamili wa njii hii hapo chini.

Kupitia kipengele hicho kipya cha ‘Last Online‘, kimewezesha watu wengine kwenye mtandao huo waweze kuona mara yako ya mwisho kutumia Instagram ilikua saa ngapi. Kwa namna fulani hii ni muhimu lakini kwa watu wengine wameiona kama ni muingiliano wa faragha. Kwenye makala hii, tumeandika jinsi ambayo mtumiaji anaweza kuzima watu kuona ‘Last Online’ na hivyo watu kutokujua mara ya mwisho kutumia mtandao huo.

Jinsi ya kuzima ‘Last Online’ kwenye Instagram

Njii hii ni rahisi na haraka unahitaji kufuata hatua chache zifuatazo

#1 Kwanza kabisa, fungua programu ya Instagram kwenye simu yako ya Androis au iOS. Hii ni muhimu kutumia programu ya kwenye smartphone yako ili kuweze kuzima ‘Last Option’. Kuna baadhi ya watu wanatumia Instagram kwenye mfumo wa kompyuta (Web version) hivyo hawataweza kuendelea na njia hii.

SOMA PIA: Facebook Messenger yaungana na PayPal kuwezesha ufanyaji malipo

#2 Sasa ingia kwenye akaunti yako ya Instagram kupitia programu na kisha nenda kwenye ‘Profile’ ndani ya programu. Hii ni rahisi kufanywa, kwa watumiaji wa Android bonyeza kitufe cha ‘Menu’. Kwa watumiaji wa iOS bonyeza kitufe cha ‘Settings’ kisha badilisha taarifa za profile ndani ya programu.

instagram-1

#3 Kwenye vifaa vyote viwili unapofika kwenye ‘Settings’ shuka chini mpaka utakapoona chaguo linaloitwa ‘Show Activity Status’. Chaguo hilo ndo litakalokuwezesha kuzima ‘Last Online’. Zima chaguo hilo na kisha save mabadiliko hayo. Hii itaondoa kipengele hicho na papo hapo wafuasi followers wataacha kuona mara yako ya mwisho kua online ilikua saa ngapi.

Hapa chini tumetengeneza video fupi kuonesha hatu hizi kwenye mtandao wa Instagram. Ni matumaini yetu itakusaidia, Asante.