Jua ‘updates’ za programu za mitandao ya kijamii kwenye simu janja

969

Kila baada ya muda, programu zote huwa zinapewa vionjo na vipengele vipya ili kutatua tatizo fulani au kuwezesha urahisi katika utumiaji wake

 

Instagram

Programu ya mtandao wa kijamii maarufu kwa kushirikiana picha na video wemeleta kipengele kipya kinachoitwa ‘poll’. Kipengele hicho kinakuruhusu ufanye uchaguzi na watu wote watakaoona picha yako kwenye ‘story’ wataweza kupiga kura kulingana na uchaguzi uliowapa. Mpaka sasa ‘instagram’ inawatumiaji takribani Mil 800

 

Twitter

Soma pia: Twitter yaongeza mara mbili kiwango cha maneno katika tweet

Mtandao wa kijamii ambayo ni maarufu kwa ujumbe mfupi chini usiozidi herufi 140, wameachia kipengele kipya cha ‘popular articles’ ambacho kinakuonyesha Makala maarufu watu walizo shirikisha kwenye ratiba ya wakati ya programu hiyo. Hadi sasa Twitter ina watumiaji tabribani Mil 328

 

 

Snapchat

Soma pia: Kua makini, iOS 11 inaruhusu watu kurekodi posts zako bila kukupa taarifa

Mtandao wa kijamii maarufu kwa watumiaji wengi kuwa na umri wa vijana, umeongeza kipengele kipya cha kuruhusu mtumiaji kurekodi video Zaidi ya moja kwa muunganisho. Hapo mwanzo ilikubidi ukimaliza kurekodi video ya sekunde 10 na utume kwenye ‘story’yako nakurudi kwenye kamera kurekodi nyingine. Sasa utarekodi video hadi 6 kwa muunganisho. Vile vile wameongeza kipengele cha ‘tint brush’ kitakacho kuwezesha kubadilisha rangi ya vitu kwenye picha yako na ikapata muonekano wa rangi mpya utayotumia na kipakio cha ‘brush’. Snapchat inawatumiaji 63% wana umri kuanzia miaka 24 kushuka chini.

 

WhatsApp

Soma Pia: WhatsApp imezuiwa matumizi nchini China, orodha ya mitandao ni zaidi ya 3,000 imezuiwa hadi sasa

Mtandao maarufu kwa utumaji wa ujumbe maneno, sauti, video, picha, GIF na faili, wamebadilishi muonekano wa ‘emoji’ zao zote. Katika toleo la  ‘WhatsApp beta’ ambalo linakuruhusu uweze kupata vipengele hivyo mapema zaidi kuliko wengine vikiwa bado katika matengenezo ya mwisho. WhatsApp kwa ina watumiaji takribani Bil 1.3, inaendelea kufanya vizuri baada ya kununuliwa na Facebook.

Tuandikie maoni yako ili tuweze kuboresha habari zetu za kila siku na pia tembelea page zetu Instagram, Twitter na Facebook @SwahiliBytes