Kampuni ya Bakhresa kuja na mtandao wa Azam Telecom

510

Sekta ya mawasiliano nchini Tanzania hivi karibuni itakua na mshindani mpya baada ya kampuni ya Bakhresa Group of Companies(BCG) kutangaza kuingia katika biashara hiyo.

Kampuni hiyo ya mawasiliano itajulikana kama Azam Telecom(T) Limited, ni sehemu ya BCG inayomilikiwa na mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania, Said Salim Bakhresa.

Mkurugenzi wa mambo ya Ushirika wa (BCG), bwana Hussein Suphian Ally, alisema: Tunaishukuru TCRA kwa kutupatia nafasi. Tuna shauku kubwa ya kuingia katika moja ya sekta yenye ushindani mkubwa nchini.

SOMA PIA: Microsoft Edge kuja na kizuia matangazo kwenye iOS na Android

Alisema Azam Telecommunications inalenga kuendeleza maono ya Bakhresa Group ya kutoa huduma bora kwa gharama nafuu kwa watu wote. Alibainishia pia kua wameshapata vibali kutoka TCRA vitakavyowezesha kutoa huduma za mawasiliano ikiwemo huduma ya intaneti yenye kasi ya 4G.