Kashfa ya Facebook yawafanya watu kama Elon Musk kufuta account zao

306

Facebook ikiendelea kupewa tuhuma nyingi kuhusiana na kutumia data za watu vibaya(Soma Facebook yapata kashfa nzito kuhusu uchaguzi mkuu wa Kenya na USA), na kusaidia kusambaza habari za uongo. Watu mashuhuri wanafuta account zao kwa kutumia neno hili #DeleteFacebook kwenye Twitter

Elon Musk alianza kwa kufata challenge ya followers wake walipomuambia afute Facebook za kampuni zake Tesla Motors na SpaceX. Akajibu hakujua kama zipo

Baada ya muda mfupi, page zote za Sola City, Tesla Motors na SpaceX zilipotea kwenye Facebook.

Soma Pia: Facebook yapata kashfa nzito kuhusu uchaguzi mkuu wa Kenya na USA

Pia mchekeshaji maarufu Will Ferrel ameacha ujumbe mrefu kwa fans wake kuhusu kufuta Facebook yake, akieleza sababu zake na kutoa masaa 72 ili watu wasome kabla hajafuta

Ukiingia Twitter na kuangia #DeleteFacebook utaona watu wengi wenye muamko wa kufuta account zao huku wakielezea sababu zinazowapelekea kufanya maamuzi hayo.

Ongea na mimi kwenye Twitter, nitakujibu!