KENYA: Itaanza kutumia maputo ya Google kusambaza huduma ya internet vijijini

207

Kenya inamkakati wa kutumia huduma ya ‘Project Loon’ kutoka kwa kampuni ya Alphabet. Mradi huo unasambaza miale ya intanet kwa kasi kubwa kwa kutumia maputo, na utawalenga wanaoishi vijijini na sehemu zisizo na huduma za intaneti nzuri

‘Projet Loon’ ni teknolojia iliyotengenezwa na kampuni mama ya Google inayoitwa Alphabet. Mradi huo unaosambaza intaneti kwa maputo yanayoelea angani na kutembea sehemu mbali mbali, ulitumika kusaidia mawasiliano ya internet huko Puerto Rico na kusaidia takribani watu 250,000 kipindi cha majanga ya kimbunga.

Mr Joe Mucheru, waziri wa habari, teknolojia na mawasiliano aliongea na Reuters siku ya jumatano kuhusu mradi huo, na kusema bado wako kwenye kumalizia mikataba.

Soma Pia: Roboti Sophia akutana na waziri mkuu wa Ethiopia

Zaidi ya watu milioni 45 Kenya ndani ya miji yote wapo kwenye mtandao mzuri, ila pia sehemu kubwa ya vijijini bado haina.

Alimalizia na kwa kusema ” Kuunganishwa na internet ni muhimu. Kama haupo online, unaachwa na mengi”

Ongea na mimi kwenye Twitter!