Kivinjari kipya kutoka Mozilla Firefox kukizidi kasi kile cha Google Chrome

803

Watumiaji wa kivinjari cha Firefox wanatakiwa kukaa mkao wa kula kwani shirika la kivinjari hicho Mozilla linazindua kivinjari kipya kiitwacho Firefox Quantum leo hii.

Kitu kikubwa kilichozungumzwa kuhusu kivinjari hicho kipya ni kasi yake ambayo Mozilla wamesema ni itakuwa mara mbili zaidi ya uwezo wa matoleo yaliyopita ya Firefox.

Licha ya kasi katika kivinjari hicho pia kuna mabadiliko mengine makubwa kwenye muonekano wake kama inavyoonekana hapo chini.

Firefox Quantum

SOMA PIA: Twitter yatambulisha herufi 280 kwa watumiaji wote

Quantum pia inakuja na mbinu mpya kwenye tabs za kwenye kivinjari hicho ambapo zitazipa vipaumbele tabs kulingana na jinsi vilivyopangwa. Kufanya hivyo itapunguza kwa asilimia 30 matumizi ya RAM kuizidi Google Chrome.

Unaweza kupata toleo la majaribio la kivinjari hicho hapa ambacho kinapatikana katika ‘platforms’ zote.