KOMPYUTA: Jinsi ya kuchagua kompyuta itakayofaa kutumia na aina za watumiaji

1735

Vitu vya kujua kabla ya kuchagua kompyuta                                              

Miaka ya 2000 na kurudi nyuma, kompyuta zilikua na muonekano mmbaya, nzito na bei ghali. Hivi karibuni utumiaji wa kompyuta umeongezeka kwa hali ya juu, na kufanya bei ishuke na matoleo yawe mengi. Kuna matoleo mengi sana, na huu uchambuzi ni kwa ajili ya mtu mwenye nia ya kununua kompyuta ila hajui ipi itamfaa.

 

1. Aina za kompyuta

Swali la msingi ni kujiuliza kompyuta unayoitaka itakua na matumizi yapi?, hamna kompyuta itakayokidhi mahitaji yote, kompyuta yenye uwezo mkubwa itanyimwa umbile dogo, na kompyuta zote zenye maumbile madogo hazipewi uwezo mkubwa. Ili usije ukanunua ambayo inapishana na matumizi yako. Nimejaribu kuelezea makundi 7 ya aina za kompyuta.

Entry-level

 

Hizi ni kompyuta ambazo ndo zina bei ndogo kutokana na matumizi yasio hitaji uwezo mkubwa, zinafaa sana kwa ajili ya kuandika dokumenti, kutumia intaneti na kuangalia movie. Kama wewe ni mpenda michezo (Video games) matoleo ya ‘entry-level’ hayata kufaa. Watumiaji wengi wake ni wasio hitaji mbwembwe nyingi.  Nyingi zina Ram GB 4 na kushuka chini, processor ya Intel Core i3, Pentium 4 au Dual Core.

 

 Nyembamba na nyepesi

Hapa ni wanapenda wepesi wa kompyuta, ambapo utakuna na ‘Ultrabook’  na MacBook Air, Dell XPS ambazo ziwepewa umbile dogo la scrini inchi 13 had chache zenye inchi 15. Bei zake ni kubwa kutokana na kupewa uwezo wa juu kidogo kuliko za ‘entry-level’ na kuwa na mvuto,diski ngumu yenye teknolojia ya SSD. Sifa yake ni rahisi kuzibeba kutokana na wepesi wake. 

 

Kompyuta mkunjo

Hizi ni laptop ambazo pia ni tablet, unaweza ukatenganisha kioo chake na keyboard na kuitumia kwa peni au kidole kwa kua ina skrini ya kuguswa. Kampuni ya Microsoft inazo zinaitwa Surface Line, Ni nzuri na zina mvuto wa hali ya juu, uwezo wake ni mkubwa pia. Ila bei yake ni kubwa, kwa wale wenye bajeti ndogo hii haitawafaa. 

 

Kompyuta za kibiashara

Zina muonekano wa kisasa kwa watumiaji wanaopenda kwenda na wakati, na kutumia teknolojia vya mwishoni zinatunza umeme kwa muda mrefu kama wewe ni mtu wa kusafiri, na zipo tayari kwa kazi nzito katika mambo ya ‘designing’. Uwezo wake wa ufanyaji kazi ni mkubwa, pia zinauzwa kwa bei ya juu. Kama unataka kuonekana ‘proffesional’ katika kazi zako hii itakufaa

 

Kompyuta zenye muonekano mkubwa

Zinajulikana kwa neon ‘Desktop replacement’ kutokana na ukubwa wa skrini (inchi 17) Na huwa sio za kuzunguka nazo kila unapoenda. Ni kwa wale wanaotaka uwezo wa kompyuta za desktop ziwe kwenye laptop. Zina sifa ya kuwa na spika zenye sauti kubwa, na kuzifanya ziwe nzuri kwenye kutoa burudani ya music na kuangalia Movie 

 

Kompyuta kwa ajili ya ‘Gaming’

Aina hii ni kwa wanaopenda michezo ya games, muonekano wa kioo umezidishwa na kupewa teknolojia ya Nvidia au AMD, ufanyaji kazi wake ni wa hali ya juu (RAM na Processor) ili kucheza games za kisasa, laptop hizi sio nzuri kusafiri zako kwa kuwa ni nzito, muonekano wake wa nje huwa sio mzuri sana kutokana na ukubwa na sio nyembamba

 

Kompyuta kwa wanaofanya ‘3D modelling’

Hizi ni aina maalum kwa kazi za 3D, ambazo viwandani na watengenezaji cinema wanatumia. Bei yake ni kubwa sana, kutokana na kuwa na teknolojia ya graphics za Nvidia Quadro. Kama una matumizi yanayo husika na 3d au 2d animation, hii itakufaa.

2. Kuhusu ‘Hardware’

Uwezo wa kompyuta unatokana na teknolojia ya vifaa inavyotumia, na jinsi vifaa vinavyokuwa na nguvu zaidi ndo bei ya kompyuta inazidi kuwa kubwa. Kampyuta ambayo itatumika mwa kuandikia dokumenti, kutembelea tovuti mbali mbali haina haja ya kuwa na teknolojia kubwa za hardware. Zifwatazo ni hardware chache ambazo ni msingi mzuri kuzijua:

Soma Pia: iPhone X: Hiki ndo kionjo kipya cha Animoji kinachopendwa sana

CPU/Processor

Kila kifaa cha kompyuta lazima kiwe na CPU, muda wowote kompyuta inapo hitaji kufanya kazi iwe ndogo au kubwa , CPU ndo inahusika. Ukiwa na CPU kubwa basi kazi xote zinafanyika kwa haraka Zaidi na kiasi kikubwa. Kwa sasa CPU ambazo zipo vizuri kwenye Soko ni  Core i3, Core i5 na Core i7 ambayo ina matolea ya mwishoni, pia kuna CPU za kampuni ya AMD. Jaribu kununua kompyuta yenye CPU ambayo toleo lake sio ya zamani zaidi ya miaka 3

 

Graphics

Kadi ya graphics ndo kifaa husika na muonekano wote wa skrini, picha na video. Mara Nyingi kadi hizo zinakua kwa ajili ya mcheza games na anaefanya 3d modelling, hufanya kazi nzuri sana. NVIDIA na AMD ndo kampuni kubwa na maarufu kwa utoaji wa kadi za graphics ingawa zinakua bei ghali. Matoleo ya mwisho ni kama GTX 1080, 1070, na 1060, AMD wana muendeleozo wa Radeon  R7 na R9. Ni vizuri kujua aina ya kadi iliyopo kwenye kompyuta kabla hujafanya maamuzi ya kununua.

 

RAM

Ni kifaa cha kutunza data za kompyuta kwa muda mfupi, kazi yeyote inayofanyika lazima itumie RAM, kwahiyo ukiwa na RAM kubwa inamaana spidi ya kufanya vitu inakuwa kubwa, kwa mfano ukiwasha kompyuta yako kama RAM yako ni kubwa basi itawaka ndani ya sekunde chache, ukifungua programu Fulani Muda mwingine inachukua dakika kibao, basi hapo ni kutokana na RAM kuwa ndogo.

Storage

Hapa unahitaji kuangalia nafasi ya diski kiendeshi ambayo inahusika na kutunza faili zako zote, na faili zinazo hitajika na kompyuta ili kufanya kazi vizuri. Ingawa kuna teknolojia ya SSD (Solid State Drive) inayowezesha ufanyaji kazi wa kasi kubwa sana kulinganisha na diski kiendeshi ya kawaida. Chagua kompyuta yenye ujazo mkubwa angalau kuanzia GB 300 kwenda juu.

 

3. Mac au PC ?

Mpaka sasa wapinzani wakubwa kwenye program kiendeshi ya kompyuta ni Apple ambao wana matoleo ya Mac na Microsoft ambao wana Windows inayo sambazwa kwenye kompyuta tofauti tofauti kama HP, Dell na Acers. Pia kuna Programu kiendeshi inayoitwa Linux, hii inapendwa na watu wachache kwa mambo ya kutengeneza programs za kompyuta na udukuzi.

Mac

  1. Apple wana program nzuri za kama Handoff, iMessage, iCloud, iCloud Drive, iCloud Photo Library, iCloud Keychain, Find My iPhone
  2. Ni rahisi kutumia kwa mtu yeyote kuliko PC
  3. Haipatagi virus sana, kwa sababu watumiaji wake ni wachache
  4. Mac zina mvuto na teknolojia nzuri Zaidi kila toleo (innovation)
  5. Kioo kinacho onyesha vizuri

PC

  1. Watengenezaji ni wengi kama HP, Dell, Toshiba, Acer na zaidi, bei zipo tofauti na nyingine chini. Mac ina tengenezwa na Apple tu kwa hiyo bei zake ni kubwa sana.
  2. PC ina nguvu zaidi, Mac ipo simple sana
  3. Inafaa kwa gaming kutokana na kuwekwa Graphics card zenye nguvu
  4. Inapata programu nyingi
  5. Ni bei ndogo kutengeneza kama ikipata tatizo

Soma Pia: UBER: Waonyesha jinsi helikopta-taxi zao za UberAir zitakavyofanya kazi

Natumaini hayo yatakupa muongozo na kujua kompyuta ipi inayofaa katika matumizi yako. Ahsante kwa kusoma, nisaidie kushare kwa marafiki na wanaoulizia kompyuta ipi ni nzuri ya kununua.