Kua makini, iOS 11 inaruhusu watu kurekodi posts zako bila kukupa taarifa

881

Wengi wetu tunafahamu Snapchat ni mtandao wa kijamii unaohakikisha usalama wa hali ya juu sana kwa watumiaji wake. Ukiachilia mbali hatua zote za kiusalama, inahakikisha kua picha zinazobadilishwa baina ya watumiaji haziwezi kuhifadhiwa. Ina mfumo wa tahadhari kuhakikisha hakuna unyanyasaji.

Snapchat ni moja ya mitandao ya kijamii inayotoa dhamana kubwa ya usalama kwa watumiaji wake. Mbali na hatua zote za ulinzi, inahakikisha picha zinazobadlishwa haziwez kuhifadhiwa kuzuia unyanyasaji.

Mfumo huu umekua ukifanya kazi vizuri hadi sasa, lakini hali imebadilika baada ya kuwasili kwa toleo jipya la mfumo wa uendesha (OS) kutoka Apple, iOS 11. Watumiaji kadhaa wameripoti kua wameweza kuhifadhi picha za watumiaji wengine bila watumiaji hao kutaarifiwa kuhusu hilo.

Ingawa bado haijajulikana sababu ya kushindwa kwa Snapchat kugundua madhaifu hayo, wengi wao wameihusisha na mfumo mpya unaowezesha mtumiaji wa iOS 11 kurekodi skrini kama sababu kuu.

Taarifa zinasema wakati wa kutumia mfumo huu mpya wa iOS 11, Snapchat haijui kua taarifa zinakamatwa inayopelekea kushindwa kutoa taarifa kwa mtumiaji kama inavyotarajiwa.

Watumiaji wengine, ambao pia wamejaribu njia hiyo wameripoti, tabia tofauti. Taarifa ilikua ikitumwa lakini baada ya muda fulani bila kujua sababu ya utofauti huo. Wengi pia wamesema tahadhari zinafanya kazi bila usahihi.

Snapchat tayari inafahamu tatizo hilo na wako mbioni kutafuta suluhisho la kudumu kwa ajili ya watumiaji wake, bila kutegemea jinsi Apple wanavyoweza kuhifadhi picha hizo.

Toleo jipya la Snpachat limeshatolewa na taarifa zinafanya kazi kama kawaida mfumo wa kurekodi skrini unapotumika. Ingawa kwa suluhisho hilo kufanya kazi watumiaji wote wawili wanatakiwa kuna toleo jipya la programu ya Snapchat kwenye simu zao.

Kama tatizo hili halitapatiwa suluhisho la kudumu, Snapchat itakua matatani ikidhihirisha kutoweza kuhifadhi taarifa za watumiaji wake, ambao ndio ulikua sababu ya msingi kuchaguliwa na watumiaji wake.

 

Ni nini maoni yako kuhusu hili, Tuachie Maoni ama ushauri  wako hapo chini!

1 COMMENT

Comments are closed.