Makampuni ya Kichina kufuatilia hisia za wafanyakazi

  227
  hisia-helmeti

  Makampuni nchini China yanaripotiwa kufuatilia hisia za wafanyakazi kwa kutumia sensa ndogo zilizowekwa chini ya kofia maalum.

  Kampuni hizo hutumia data zilizokusanywa kutoka kwenye kofia ili kutambua msongo wa mawazo(stress), sonona (depression), na masuala mengine ambayo yanaathiri utendaji wa wafanyakazi.
  Ikiwa suala lolote limegunduliwa, mfanyakazi atapewa ruhusa ya kwenda kupumzika nyumbani au mtumishi huyo atahamishwa kufanya kazi katika idara nyingine ambako kazi si nyingi sana.

  SOMA PIA: Instagram yazindua programu ya IGTV kwa watumiaji

  Hangzhou Zhongheng Electric ni moja ya makampuni mengi ambayo hutumia helmeti hizi. Na wanasema kuwa kifaa hiki kimebuniwa kuongeza ufanisi wa kazi kwa jumla. Wao wamethibitisha kuwa teknolojia hii ilifanya kampuni yao kuzalisha zaidi.Teknolojia hii imeongeza ukaribu zaidi kati ya wafanyakazi na waajiri wao.

  Hangzhou Zhongheng Electric walisema kuwa helmeti zilibuniwa hasa kutumika kuwafundisha wafanyakazi wapya. Ingawa hawakuwa na maoni juu ya kama helmeti zilitumiwa tu na wafanyakazi wapya, hata hivyo.