Mambo 20 Usiyoyajua na Kushangaza Kuhusu Teknolojia

162

Mambo haya 20 yanaacha watu kwenye mshangao, yasiyotegemewa na kuchekesha wengine kutokana na kutodhaniwa katika teknolojia.

 1. Kompyuta zilijulikana kwa jina la “Electronics Brains” miaka ya 1950
 2. Barua pepe zimekuwepo kwa muda mrefu sana zaidi ya WWW (World Wide Web)
 3. Hp, Google, Microsoft na Apple wote wana kitu kimoja sawa, walianza biashara zao kwenye karakana (Garage)
 4. Nyumba ya tajiri Bill Gates ilibuniwa kwa kutumia kompyuta ya Mac kutoka Apple na sio za kampuni yake Microsoft
 5. Kuna karibuni virusi 6,000 vya kompyuta vipya kila mwezi
 6. Utengeneza wa programu za kompyuta (Programming) ndo kazi inayokua kwa kasi katika teknolojia kuliko zote
 7. Asilimia 28% ya wanaojua IT huficha taaluma zao kwa marafiki na ndugu ili wasiombwe misaada ya bure kuhusu kompyuta na IT kwa ujumla
 8. Tarehe 30 ya mwezi novemba ni siku ya usalama wa kompyuta (Computer Security Day)
 9. Technophobia ni hofu ya teknolojia, Nomophobia ni hofu ya kutokua na simu, Cyberphobia ni hofu ya kompyuta
 10. Jina la kwanza la kompyuta za “Windows” ilikua ni Interface Manager
 11. Intanet ina umri wa siku 10,000 na zaidi. Tembelea hapa kujua hadi siku kwa uhakika
 12. Kibodi ya kompyuta aina ya QWERTY ilibuniwa kupunguza spidi ya mwandishi, zamani ukiandika kwa spidi kubwa unaleta tatizo kwenye kifaa unachotumia
 13. Hadi sasa, hard drive kubwa inafika Terabyte 60TB katika aina ya SSD
 14. Toleo la kompyuta ya Apple 2 ya mwaka 1977 ilikua na hard drive yenye ukubwa wa 5MB tu
 15. Asilimia 51% ya trafiki ya intaneti sio binadamu, asilimia 31% ni programu za udukuzi na spamming
 16. Kompyuta ya kwanza ilikua na urefu wa mita 2.5 na uzito wa kilo 30,000
 17. Jina ‘Google’ lilipatikana kwa bahati mbaya, baada ya Larry Page na Sergey Brin kukosea kuandika Googol
 18. Mtu wa kawaida anafumba macho mara 7 kwa kila dakika akiwa anatumia kompyuta, ni chini ya kawaida ambayo binadamu anatakiwa ni mara 20.
 19. Mouse ya kompyuta ya kwanza iliundwa na Doug Engelbart na ilitengenezwa kwa mbao
 20. Jarida maarufu la TIME, liliandika kompyuta ni mwanaume wa mwaka 1982.

Soma Pia: Vipengele 10 vya muhimu kwenye iOS 12 inayokuja hivi karibuni

Ongea na mimi kwenye Twitter!