Mapacha waliomshtaki Zuckerberg watajwa kuwa mabilionea wa Bitcoin

1277

Unakumbuka wale mapacha waliomshtaki Mark Zuckerberg kwa kudai aliiba wazo lao la kuanzisha mtandao wa Facebook? Mapacha hao kutoka familia ya Winklevoss sasa watajwa kuwa mabilionea wa bitcoin.

Cameron na Tyler Winklevoss walishinda fedha kiasi cha dola za Kimarekani milioni 65 katika mashtaka dhidi ya Zuckerberg na wakaamua kuwekeza kiasi cha dola za Kimarekani milioni 11 kwenye Bitcoin mnamo mwaka 2013.

SOMA PIA: Net Neutrality: Uhuru wa utumiaji internet upo HATARINI

Mnamo mwaka huo mapacha hao walinunua bitcoins zipatazo 10,000 huku wakati huo zikiuzwa moja kwa dola 1000 za Kimarekani. Tangu hapo, mauzo ya bitcoins yamepanda zaidi ya mara kumi na kufikia dola 11,310 ambayo ndio bei yake ya sasa.

Mapacha hao wametajwa kuwa mabilionea katika mfumo huo wa kifedha kupitia mtandao kutokana na kuongezeka huko maradufu kwa mauzo ya bitcoins.