Mapya yote ya teknolojia yaliyotajwa na Google kwenye tukio la ‘Pixel 2’

956

Kama hukupata nafasi ya kuangalia tukio la ‘Google – Pixel 2’, Swahilibytes inakufahamisha yote mapya ambayo yalitangazwa hapo jana Oktoba 4.

 

Google Pixel 2 & Pixel 2XL

Kama ilivyo kawaida ya Google kuleta toleo jipya la simu janja zao zinazojulikana kwa jina la ‘Google Pixel’. Wametangaza toleo la Google Pixel 2 na Google Pixel 2XL ambazo zinatofautiana kwa ukubwa wa muonekano. Simu hizi janja zina muongozo wa ‘Google Assistant’ ambayo inakupa urahisi wa kutumia simu ya intanet kuliko simu zote. Wameleta uwezo mpya wa simu hizo inaitwa ‘active edge’ na kazi yake ni kukuletea msaada wa Google pale unapo kandamiza kwenye upande wa kushoto na kulia kwa mkono ulioshikilia simu hizo, na utaweza amrisha simu janja hizo kwa sauti.

 

Google Pixelbook

Kompyuta nyembamba zaidi na nyepesi, ambayo inatumia programu muendesho wa ‘Chrome OS’. Imepewa muongozo wa ‘Google Assistant’ kama simu zote za Google, na bila kusahau itakua na kalamu ya digitali ‘Stylus’  inayoitwa ‘Pixelbook Pen’ itakayo kusaidia kutumia kwa urahisi kompyuta hiyo.

 Google Home Max

Nani asiyependa mfumo wa sauti kusikilizia muziki?

Vile vile wakaonyesha mfumo mpya wa sauti ambao una ubora wa hali ya juu kwa mara 20 kulinganisha na toleo lao la mwaka jana ‘Google Home’. Ina spika mbila kubwa za kukita sauti kwa hali juu, utaweza kuunganisha na programu za burudani kama Spotify, YouTube Music, Pandora, Google Play, TuneIn, iHeart Radio na zinginezo maarufu. Google Home Max itashindana na matoleo ya Amazon Echo na HomePod za kampuni ya Amazon na Apple katika soko la mfumo wa sauti ndani ya nyumba.

 Google Home Mini

Kuna kitu kikubwa bila kidogo chake?

Mfumo wa sauti huu ni mdogo wake ‘Google Home Max’, unaumbile dogo na kukusaidia kujibu maswali yote utakayo uliza na kuweka ‘alarm’ kuuliza ramani na umbali wa sehemu zote, hali ya hewa na maswali yote ambayo ungependa ‘Google’ikupe majibu kwa sauti ya mdada.

 

 Google Pixel Buds

Katika vitu vilivyofurahisha watu ni ‘earphones’ mpya ambazo zitakupa uwezo wa kutafasiri lugha 40 kubwa. Wakati mtu anaongeana wewe, Pixel Buds zitatafsiri anachoongea kwenye masikio yako. Zitakua hazitumii waya wowote ‘wireless’ na kustahimili masaa 5 bila kuweka chaji ya umeme.

 

Soma pia: Kua makini, iOS 11 inaruhusu watu kurekodi posts zako bila kukupa taarifa

Google Clips

Bila kusahau kamera

Google Clips ni kamera ndogo itakayokusaidia kuchukua picha za kumbukumbu katika kila siku yako. Imekewa teknolojia ya ‘artificial intelligence’ ya kujua muda wa kupiga picha nzuri bila kubonyeza kitufe cha kupigia, ni nyepesi na itatunza picha zako kwenye program ya ‘drive’ ambayo inakupa nafasi ya GB 15 za bure.

 

Ni mengi yalielezwa na Google, SwahiliBytes tutaendelea kutoa mfupisho wa ‘events’ zote za teknolojia zinazojalisha. Usisahau kuandika maoni yako na kushare kwa marafiki, Thanks.