Njia rahisi ya kupunguza faili nyingi kwenye kompyuta iliyojaa

1092

Je? kompyuta yako imekua inachukua muda mrefu kuwaka hadi kufika kwenye muonekano wa mwisho, au umekua unapata ujumbe mfupi ukikujulisha upunguze faili.

Kuna njia chache kuu utakazoweza kutumia kufanikisha upunguzaji wa mafaili. Pengine huna haja ya kwenda kwa fundi na kutumia gharama wakati ni njia unazoweza kuzifata ukiwa umetulia kwenye kiti na chai yako pembeni. Kitu cha kuzingatia ni vizuri ukatunza faili za muhimu kwenye ‘backup’, ili usije ukafuta kwa bahati mbaya, SwahiliBytes haitahusika kwenye upotevu huo.

Fungua ‘Disk Cleanup’

Hii ni programu inayakuja na kompyuta yako (Windows), na kazi yake ya msingi ni kufuta vitu ambavyo havihitajiki. Kama ilivyo kwenye picha chini, ukifata hatua chache zitakusaidia kupunguza faili usiohitajika.

 

Futa %temp%

Njia hii inatumika na wachache sana, ila ni muhimu kuitumia kila baada ya wiki kadhaa. Inasaidia kutoa mafaili  ‘temporary’ ambayo huhitajika kwa muda mfupi na kisha hubaki yakirundikana. Kompyuta yako ikiwa imewashwa bonyeza vitufe vya ‘windows + R’ kwa pamoja  kama kwenye picha chini na kisha andika %temp% ikifuatiwa na kubofya kitufe cha ‘Enter’. Futa kila kitu utakachokikuta. Hapo utakua umepunguza mzigo wa komputya, Mimi leo asubuhi nimepunguza kiasi cha ‘7GB’.

Bofya kwa pamoja 'Windows + R'
Bofya kwa pamoja ‘Windows + R’

 

 

Futa Programu (Applications) Usizozitumia

Ni mara ngapi unaweka programu ambazo ungependa kuzijaribu uone zinatumika vipi na kisha unasahau kuzitoa? basi moja wapo ya kujaa kwa kompyuta yako na kuifanya iwe inawaka kwa spidi ndogo sana ni mlundikano wa programu. Fuata hizi hatua chache kwenye picha ili ujue jinsi ya kuzitoa.

baada ya hapo utaonyeshwa orodha ya programu zote ndani ya kompyuta yako, chagua ambazo huzitumii na kuzitoa kwenye ‘uninstall’.

Tumia programu za usafishaji

Ikiwa ungependa msaada wa programu yakufanya kila kitu kwa pamoja, napenda kukushauri utumie programu zilizopo hapo chini ni rahisi kutumia na itakuletea sehemu zote za kupunguza vitu vyote kwa pamoja. Bofya moja wapo kwenda kuangalia kama itakufaa kwa matumizi yako.

 

Ahsante kwa kusoma, kama una swali au maoni andika tutakujibu. Usisahau kushare kwa watakaohitaji maujanja kama haya.

1 COMMENT

Comments are closed.