Maujuzi: Jinsi ya kutuma faili kati ya simu na kompyuta kwa spidi kubwa zaidi ya kutumia USB cable

1154

Mara nyingi ukihitaji faili la movie au dokumenti kubwa unatumia njia ya kawaida na inayofahamika kila sehemu ya waya wa USB na kuchomeka kwenye simu na kompyuta na kuhamisha. Pia njia hii huwa ina spidi ndogo

Kama una movie unataka kuangalia kwenye simu basi utasubiri sana ukitumia bluetooth au cable. Leo nimekuletea njia rahisi ya kuhamisha

Njia hii utahamisha kwa kutumia Wi-fi ya simu na kompyuta ambayo spidi yake ni kubwa  kulinganisha na Bluetooth na USB cable.

Tembelea tovuti ya shareit na upakua programu ya simu yako android au iOS, na kisha pakua programu ya kompyuta Windows au Mac

Soma Pia:

  1.  Maujuzi: Jinsi ya kuangalia movie mtandaoni bila kuipakua
  2. Apple watoa orodha ya Apps zinazoongoza kwa ubora mwaka 2017

Install kwenye vifaa vyako, kisha itakupa maelekezo ya jinsi ya kutuma au kupokea faili, hakikisha simu yako ina nafasi ya kupokea faili unazotaka kutuma kutoka kwenye kompyuta au simu nyingine.

Programu nyingine nzuri ni;

1. izapya

2. filedropme

 

Tuachie maoni yako, au swali. Ahsante!