Mionzi ya simu janja na saratani ya ubongo, uchunguzi mpya

871
Simu janja na saratani

Kuna hoja nyingi kuhusu kama mionzi ya simu inaleta saratani, hasa saratani ya ubongo. Kutokana na utumiaji mwingi wa simu karibu na nyuso zetu

Ni kweli simu zina mionzi, ila aina ya mionzi hiyo inaitwa ‘Radiofrequency radiation’, ambayo haina nguvu kama ‘ionizing radioation’ unayopata kama vile ukipiga X-Ray. ‘ionizing radioation’ inaweza leta uaribifu wa DNA na kuleta saratani. Ila mionzi ya simu janja haifanyi hivyo, repoti za uchunguzi nimefafanua

Repoti moja imeeleza kua panya wa kiume alipo wekwa karibu na mionzi kwa hali ya juu alipata uvimbe kwenye moyo, lakini panya wa kike hakupata. Katika jaribio la pili panya wote walionyesha afya njema, ingawa repoti zote bado zinaendelea.

Shirika la Federal Communication Commission linalo husika na kuendesha sheria za mawasiliano yote limeweka kipimo cha utumiaji wa mionzi inayotoka kwenye simu janja zote duniani. shirika hilo linamini kipimo hicho kipo salama kwa matumizi ya simu janja kutokana na utafiti waliofanya.

Soma Pia:

1. Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kuchaji smartphone yako

2. China yatuhumiwa kufanya udukuzi kwa Umoja wa Afrika

Uchunguzi huo umefanyika kwa kutumia mtandao wa 2G na 3G, walichukua panya hao na kuwaweka karibu na mionzi hiyo zaidi ya saa 9 kila siku kwa miaka 2 ( panya wa miaka 2 ni kama binadamu mwenye miaka 70). mionzi hiyo ilikua kwa kiasi kikubwa kuliko tunayopata kwenye simu janja. Lakini bado haikuonekana kama mionzi ya simu janja inaleta saratani yeyote, usiwe na hofu unapotumia simu janja.

Tuachie maoni yako hapo chini