Microsoft Edge kuja na kizuia matangazo kwenye iOS na Android

226
Microsoft Edge

Shirika kubwa duniani Microsoft limetengeneza kizuia matangazo (adblocker) cha moja kwa moja katika kivinjari cha Microsoft Edge kwa watumiaji wa iOS na Android.

Kizuia matangazo hicho kimeanza kufanyiwa majaribio wikiendi hii kwa watumiaji wa Microsoft Edge beta kwenye Android.

Kipengele hicho kitaanza kutumika rasmi kwa watumiaji wote wa iOS pamoja na Android hivi karibuni na kitaweza kutumika moja kwa moja kupitia mipangilio (settings) ya Microsoft Edge, hivyo haitohitaji kupakua kukipata kipengele hicho.

SOMA PIA: Vinjari kwa simu janja yako bila matangazo yanayokera (Ads)

Hatua hiyo ya Microsoft imetajwa kuwa ni kubwa katika ulimwengu wa kimtandao kutokana na kuweza kushirikiana na Adblock Plus kuwezesha matumizi yake ya moja kwa moja kupitia kivinjari cha Edge.

Google nayo ilitangaza kutengeneza kizuia matangazo chake katika kivinjari cha Chrome kwa watumiaji wa Android lakini kimeonekana kutofanya kazi yake ipasavyo kama Adblock Plus kutokana na kushindwa kuzuia matangazo yote.