Microsoft Edge sasa kupatikana kwa watumiaji wa Android na iOS

1375
Microsoft Edge kwa Android na iOS

Mnamo mwezi uliopita Microsoft walitangaza nia yao ya kukileta kivinjari cha Edge kwa watumiaji wa Android na iOS ili kuweza kufikia watumiaji wengi zaidi.

Mara baada ya kutangaza nia hiyo Microsoft waliachia kivinjari hicho kwa majaribio kwa watumiaji hao wa Android na iOS, na sasa rasmi kupatikana kwenye hifadhi/store za platforms hizo mbili.

Soma Pia: Kivinjari kipya kutoka Mozilla Firefox kukizidi kasi kile cha Google Chrome

Kivinjari cha Edge kimepata mafanikio mengi tangu kuanzishwa kwake katika mfumo wa Windows 10 na kutoa machungu ya watu wengi waliokuwa wakikilalamikia kwa muda mrefu kivinjari cha hapo mwanzo Internet Explorer.

Kupatikana kwa kivinjari Edge katika iOS na Android ni mkakati mzuri kutoka Microsoft hususani baada ya kukubali kushindwa katika sekta ya simu janja.