Microsoft kumpa vifaa mwalimu wa Ghana anaefundisha kompyuta ubaoni

860
mwalimu ghana akitumia ubao kufundisha kompyuta

Baada ya kuposti picha kwenye mitandao ya kijamii, Mwalimu wa ICT kutoka nchi ya Ghana akiwa anafundisha somo la kompyuta ubaoni, Microsoft itampatia vifaa vya kufundishia vizuri soma la ICT

Mitandao ya kijami imekuwa na uwezo mkubwa wa kusambaza mambo kwa muda mfupi. Mwalimu Richard alituma picha hiyo kwenye Facebook yake, ndani ya masaa machache afrika nzima inamzungumzia, huku wakishare picha yake na kuonyeshwa kuguswa. Kwani sio kawaida kuchora kwenye ubao muonekano wa programu ya Microsoft Word na kufundishia ubaoni.

Alivyo hojiwa alisema haya ” Hii sio mara yangu ya kwanza kuchora hivyo, ninafanya hivyo muda wowote nikiwa darasani. Pia napenda kutuma picha kwenye Facebook, ila sikujua kama picha hiyo itapata umaarufu huo”

Kwenye Facebook anatumia jina la “Owura Kwadwo Hottish” na hilo ndo jina limesambaa kwenye mitandao ya Twitter na Facebook ikiambatana na picha akifundisha ubaoni.

Baada ya kusambaa sana, Rebecca Enonchong alituma ujumbe kwa kutumia Twitter na kuwaambia kampuni ya Microsoft waweze kumpa vifaa vya kufundishia. Microsoft wajibu na kukubali ombi hilo.Akoto alielezea kwamba anayo laptop yake ilahaifai kufundishia, kwani kwenye mtaala wa kufundishia inamuhitaji mwanafunzi ajue kompyuta nzima na vifaa vyote na jinsi ya kuwasha, ila ukileta laptop darasani haionyeshi hivyo vyote.

Soma Pia:

1. TTCL yazindua huduma mpya ya internet kwa matumizi ya nyumbani

2. Vivo yawapiku Apple na Samsung, teknolojia ya fingerprint

3. Samsung warekebisha muonekano wa ‘Emoji’ zake kwenye Android Oreo