Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kuchaji smartphone yako

1200

Leo zaidi ya mabilioni ya watu wanatumia simu janja zenye mifumo ya Android au iOS. Kila mtu hukutana na tatizo la kuimarisha betri. Mfumo wa uendeshaji wa Android hutumia betri nyingi ukilinganisha na wengine.

Kwa wastani, betri zetu za smartphone zinadumu kwa saa 7-8. Betri inayodumu muda mrefu daima ni jambo la muhimu kuchunguza kwa mnunuaji yeyote wa simu janja mpaka leo.
Hata hivyo kuna tabia chache ambazo unaweza kuzitekeleza katika maisha yako ya kila siku ambazo zinaweza kusaidia kudumu maradufu kwa betri yako ya simu. Kwenye makala hii tutawakilisha vidokezo vichache vya jinsi ya kuchaji simu yako na kuifanya betri yako idumu muda mrefu.

#1 Chaji simu yako na chaji original
Itakua bora zaidi ukichaji simu yako na chaji yake yenyewe. Mara nyingi kutokana na kutingwa na shughuli zetu za kila siku hua tunasahau kubeba chaja original ya simu na kuibadilisha na chaja mmbadala. Hii inachangia zaidi kuathiri utendaji wa betri zetu. Ikiwa unatumia chaja mmbadala hakikisha output voltage( Voltage) na current (Ampere) zinafanana na chaja original.

#2 Epuka Fast Chargers
Fast charger zinaweza kua sio chaguo bora la kwa afya ujumla ya betri yako. Kuchaji simu janja yako kwa Fast chargers kunaweza kusababisha kuharibika kwa betri yako ukiitumia kwa kipindi kirefu. Kutumia fast chargers kunahusisha kuingiza voltage ya juu kwenye simu yako ambayo itapelekea joto la juu. Hivyo hakikisha kuepuka kutumia Fast Chargers.

#3 Ondoa kava la simu unapochaji simu yako
Unaweza kuwa umegundua, wakati simu zetu zipo kwenye chaji, zinakuwa na joto kidogo. Kwa hivyo, hakikisha kuondoa kava la kinga ya simu wakati wa kuchaji. Kava linaweza kua kizuizi cha joto kutoka kwenye simu. Ikiwezekana igeuze simu yako juu chini wakati unachaji.

#4 Usiache simu yako ikichaji usiku kucha
Kuna watu wengi, (nikiwemo mimi) ambao huacha simu zao zikichaji usiku mzima. Tunahitaji kuacha kufanya hivi. Kuchaji simu usiku mzima huathiri uhai wa betri, na pia hufanya smartphone yako kupata sana joto. Hivyo hakikisha kuchomoa simu yako unapohisi kuwa imepata chaji ya kutosha.

#5 Epuka programu za ziada za betri
Usitumie programu za betri za ziada (third party) kwa sababu daima zinafanya kazi kwenye background na kusababisha betri ya simu yako kuisha haraka sana na pia zinazuia programu zingine kufanya kazi vizuri. Jaribu kuepuka programu hizo zinazodai zinaongeza betri.

#6 Epuka kucheza Games kwenye simu yako
Kila mtu anapenda kucheza games kwenye simu zao za mkononi. Hata hivyo, ikiwa games ni sababu kuu ya kupungua kwa betri yako, basi unapaswa kuacha kucheza michezo wakati unachaji simu yako. Hii si tu itasaidia simu yako kujaa haraka bali itaondoa matatio ya simu kupata sana joto.

#7 Daima chaji simu yako hadi kufikia 80%
Tunapaswa kukubali kwamba 80% ya chaji ni ya kutosha kwa siku, na ni bora kwa maisha ya betri. Kuvuka alama ya asilimia 80 kunaweza kufanya betri yako kupata joto, na hivyo kuathiri maisha ya betri. Kwa hiyo, sio lazima kwamba smartphone yako iwe imefikia kiwango cha juu(100%)

#8 Epuka kuchaji simu yako mara kwa mara
Mara nyingi watu hupendelea kuchaji simu zao inapokaribia alama ya betri ya 50%. Hata hivyo, hilo sio jambo bora la kufanya. Unatakiwa kuruhusu betri kufikia karibu 20% kabla ya kuchaji tena. Uchunguzi umedhihirisha kuchaji kwa simu kusipokua na umuhimu na mara kwa mara, hufupisha maisha ya betri ya simu.

Haya ni mambo nane ya kawaida ambayo haipaswi kufanya wakati wa kuchaji smartphone yako. Kwa hiyo, hakikisha kuepuka makosa haya ili kuboresha maisha ya betri yako.

Tunatumaini umependa makala hii, share na marafiki zako pia! Asante