Mwanafunzi Kenya aunda gari la nishati ya umeme wa jua

362

Mwanafunzi mmoja nchini Kenya ameongezeka katika list ya wavumbuzi wa hivi karibuni wa magari ya nishati ya jua na uvumbuzi huo umekua kivutio katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Samuel Karumbo, mwenye umri wa miaka 30, ambaye ni mwanafunzi wa chuo cha Kitale Polytechnic, amevumbua gari hilo katika mji wa Langas Eldoret. Gari hiyo yenye siti mbili na matairi manne lina jopo(panel) la nishati ya jua kwa nyuma.

SOMA PIA: Tigo yaungana na Selcom na Mastercard kuleta huduma ya Mastercard QR Tanzania

Baadhi ya taarifa za gari hilo ni pamoja na: Kutoa 0% ya uchafuzi wa mazingira, Jina la gari hilo ni SOLAR CAR.Gari hilo linasemekana kuwa na uwezo wa kutembea kufikia kilomita 50 kwa siku likiwa limejaa chaji.

Karibu mwaka mmoja uliopita, uvumbuzi kama huu ulifanyika na wanafunzi wa chuo kikuu cha uhandisi wa Ghana, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia ya Kwame Nkrumah (KNUST) kilichoko katika mkoa wa tajiri wa rasilimali wa Ashanti.