Net Neutrality: Uhuru wa utumiaji internet upo HATARINI, Desemba 14

1362

Uwepo wa ‘Net Neutrality’ unakufanya kutumia internet yako kutembelea tovuti yeyote unayotaka, kutumia programu yeyote na kupakua vitu vyote bila kuzuiwa na kampuni za mawasiliano, kila baada ya kununua data za intaneti unapewa uhuru huo. Sasa hilo lipo katika kuzuiwa lisiendelee, hapo desemba 14 itaamuliwa kwa nchi ya marekani

Mwenyekiti wa kampuni ya Federal Communications Commission huko marekani inayohusika na sheria za uendeshaji wa mawasiliano yote nchini marekani, Ajit Pai amepitisha hoja hiyo ya kusimamia uhuru wa internet kila inapobidi. Hoja hiyo itapigiwa kura mnamo tarehe 14 ya Desemba kama ifanyiwe kazi na serikali ya raisi Donald Trump au ipuuziwe.

Hasara yake itakua ni kubwa, baada ya muda kupita uwezekazo wa dunia nzima kufata mfano huo wa marekani ni mkubwa. Itazuia ushindani wa kibiashara, kwani kampuni zitaweza kuzuia spidi ya internet kwa washindani wao na kuruhusu wanaolipia kupata spidi kubwa, au kublock kabisa tovuti yeyote inayopinga malengo yao. Uhuru wa kuongea utapungua kutokana na watu kunyimwa uhuru wa kutembelea tovuti yeyote. Utawekewa vifurushi vya utumiaji wa intaneti, kwa mfano bundle ya Youtube tu hutaweza kuingia kwenye mtandao wa kijamii hadi ununue bundle yake pia. Tembelea savetheinternet kusoma zaidi.

Nini maoni yako kuhusu hilo? Ahsante.

Soma Pia:

  1. KOMPYUTA: Jinsi ya kuchagua kompyuta itakayofaa kutumia na aina za watumiaji
  2. Facebook yatengeneza toleo lingine la Messenger kwa ajili ya watoto
  3. Maujuzi: Jinsi ya kuangalia movie mtandaoni bila kuipakua