Netflix yapanda thamani maradufu, yavuka kiasi cha dola bilioni 100

  839
  netflix logo

  Kampuni ya Netflix imepiga hatua kubwa na muhimu kimasoko leo kwa kupita kiwango cha thamani ya dola za Kimarekani bilioni 100 ($100 bil).

  Licha ya kupanda kwa thamani hiyo ya kifedha, Netflix pia imeripotiwa kujikusanyia idadi kubwa ya wanachama katika kipindi chote cha mwaka 2017.

  Imesemekana kampuni hiyo ilijikusanyia idadi ya zaidi ya wanachama milioni 8 ambapo milioni 6 kati yao iliwakusanya katika kipindi cha mwezi October mpaka December, kipindi ambacho iliachia show maarufu “Stranger Things” na “The Crown” pamoja na filamu ya Will Smith iitwayo “Bright.”

  Hakika ongezeko la idadi ya wanachama katika kituo hicho cha huduma ya televisheni online limekuwa ni chachu ya kupanda huko kwa thamani.