Njia rahisi ya kupakua filamu moja kwa moja

1460

Watu wengi tunapenda kuangalia sinema kwenye kompyuta, simu janja, na televisheni zetu — Lakini tunapoamua kutafuta sinema kwa ajili ya kupakua Google mara nyingi hukutana na kurasa zenye matangazo mengi au hata kurasa zenye maudhui yanayoweza kudhuru vifaa vyetu kama virusi.

Leo tutakuonesha njia rahisi ya kupakua sinema bila kupitia kurasa nyingi mtandaoni, njia hii itakusaidia kupakua filamu yoyote kwa urahisi zaidi. Tutatumia utafutaji wa Google tu kukuwezesha kukamilisha hili.

Njia rahisi ya kupakua filamu moja kwa moja

Njia hii ni rahisi na ya haraka, unachohitaji ni kufata hatua hizi fupi tu. Hiki ndo unachotakiwa kufanya

  1. Nenda kwenye kivinjari(browser) chochote unachotumia mf. Google Chrome, Firefox, Microsoft Edge nk. Na fungua kurasa ya Google
  2. Sasa andika jina la sinema yoyote unayotaka kupakua ikifuatiwa na code iliyopo chini

Jina la sinema  -inurl:(htm|html|php|pls|txt) intitle:index.of “last modified” (mp4|wma|aac|avi)

Kwa mf: Pirates of the Caribbean -inurl:(htm|html|php|pls|txt) intitle:index.of “last modified” (mp4|wma|aac|avi)

3. Google italeta matokeo ya utafutaji utachagua kati ya linki zilizorejeshwa na Google kama majibu na ifungue.

4. Angalia link ya sinema unayoihitaji, ifungue na itaanza kupakua!

 

Njia nyingine

  1. Nenda kwenye kivinjari(browser) chochote unachotumia mf. Google Chrome, Firefox, Microsoft Edge nk. Na fungua kurasa ya Google.
  2. Kisha nakili (copy) na andika code iliyopo hapa chini ikifuatiwa na jina la sinema unayotaka kudownload na kisha tafuta

    intitle:index.of? mkv 

Kwa Mf: intitle:index.of? mkv Sleepless

3. Google italeta matokeo ya utafutaji wako utachagua kati ya linki zilizorejeshwa na Google kama majibu na ifungue na kisha chagua linki ya filamu yako itaanza kudownload.

Angalizo: Unaweza kubadili *mkv kwenda format yoyote unayohitaji kudownload mfano mp4 na kadhalika.

 

Hiyo ndio ilikua njia ya kudownload sinema kirahisi, Naamini umeoiona makala hii ikikusaidia siku za usoni. Share na watu wengine pia waweze kujifunza njia hii. 

Kama una maswali au maoni yoyote kuhusu Teknolojia usisite kutuachia hapo chini.